Rukia hadi maudhui
Watusmart Printing Solutions

Fahamu mambo ma 3 Kabla ya kuprint mifuko ya kuweka unga .

Fahamu mambo ma 3 Kabla ya kuprint mifuko ya kuweka unga .
Katika kuhakikisha kazi yako inakuwa safi na nadhifu kabisa. #watusmartpackaging tunajuza leo mambo muhimu kabla ya kuchapisha mifuko toka kwetu au sehemu nyingine. 1. Artwork /picha Kabla ya kuchapisha mifuko ya kuwekea unga ile ya viroba au ya salfeti ni muhimu kuwa na mchoro au picha ambayo unataka kuiweka kwenye mfuko wako. Mara nyingi tunashauri iwe (softcopy)ambayo tutaweza kuitumia kufanyia marekebisho au ushauri kulingana na mashine zetu. 2. Kuichonga rubber, kazi hufanywa na wataalam ambayo kwa uhalisia kwetu #watusmartpackaging tunachukua siku 2 mpaka 3 kuikamilisha kazi ya kuchonga rubber au muhuri ambayo ndio hutumika kuchapishia viroba au salfeti. Mwisho wa posti hii ziko picha zinazoonesha hii rubber baada ya kuchongwa toka kwenye picha hadi kuwa rubber iliyo na mchoro. 3. Kuchapisha au kuprint mifuko Hatua hii ndio hatua ya mwisho na ndio kusudio letu. Na kwa hapa tunachukua siku 1 mpaka mbili kukamilisha kazi ya kuchapisha kwa maana ya kutegemea oda za siku husika na malighafi tulizonazo stoo. Hivyo kwa jibu rahisi katika swali "Lini mnamaliza kazi yangu ya kuchapisha mifuko?" Jibu : Ndani ya siku 4 mpaka 5 kwa mteja ambaye hana rubber (ndio anaanza)ila kwa yule mzoefu basi ndani ya siku moja mpaka mbili. < WATUSMART PACKAGING>